Kiswahili

Kuhusu Better-iS

Better-iS inalenga katika kutambua fursa zilizopo kwa kuunganisha kilimo kisicho na tija kwenye masoko hasa makampuni ya biashara za kati na ndogo ili kuleta tija katika sekta ya kilimo kwa kupitia fursa zinazoweza kupatikana katika shughuli za uanzishaji kilimo cha mazao ya nishati, usindikaji na matumizi ya nishati ya mimea. Uzalishaji na usindikaji wa mazao ya nishati unaolenga wakulima wadogo wa mkoa wa Morogoro ambao watakuwa wameunganishwa kwenye masoko hasa viwanda vya kati na vidogo unategemewa kuboreka zaidi. Kwa kuzingatia hali ya kuwepo kwa ongezeko la matumizi ya nishati kadri siku zinavyokwenda, mikakati ya kuwawezesha wakulima wadogo kuzalisha mazao ya nishati katika maeneo ya vijijini inaweza kusaidia katika kupatikana kwa nishati ya umeme, pia kwa matumizi ya nyumbani kama vile kupikia, kupasha joto na mengineyo, hali kadhalika mazao hayo ya nishati yanaweza kuuzwa katika masoko ya nje na kuingiza fedha za kigeni. Zifuatazo ni tathimini zitakazo fanyika ili kuweza kutambua fursa zilizopo ambazo zitawezesha kutimiza lengo.

 1. Kufanya tathimini ya jinsi mabadiliko ya hali ya hewa duniani yanavyoweza kuwa na athari kwenye ngazi ya chini katika maeneo kadhaa nchini Tanzania ambapo utafiti utafanyika ili kutambua fursa zilizopo.
 2. Tathimini shirikishi itakayo ainisha fursa zitakazo patikana kwa kuwaunganisha wakulima wadogo kwenye masoko hasa makampuni ya biashara za kati na ndogo.

Mbali na manufaa ya kielemu, wakulima, mashirika na mamlaka za serikali kusini mwa jangwa la Sahara zitaweza kuandaa mikakati madhubuti itakayo wezesha wakulima wadodo kunufaika na uzalishaji wa mazao ya nishati na kukabiliana na upungufu wa chakula.

Baada ya miaka mitatu mradi utakuwa umekamilisha mambo yafuatayo.

 • Upembuzi utakao ainisha athari zitokanazo na ongezeko la mahitaji ya nishati duniani, upatikani uliokithiri wa nishati au upungufu wa nishati.
 • Tathimini ya uzalishaji wa nishati itokanayo na mimea pamoja na matumizi ya mazao hayo kwa kuzingatia matumizi mengine (kama vile, chakula, malighafi, nishati) na jinsi ambavyo mazao hayo yanaweza kutumika kukithi mahitaji ya nishati na matumizi mengine kwa pamoja.
 • Uwiano kati ya ongezeko la mahitaji ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa unao unganisha matokeo ya upembuzi ambao unalenga katika kuainisha athari kwa nchi zinazoendelea zitokanazo na madiliko ya hali ya hewa na ongezeko la mahitaji ya nishati duniani na jinsi nchi hizi zinavyoweza kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia fursa zinazojitokeza.
 • Tathimini kuanzia ngazi ya chini kwa wakulima inayolenga katika kuangalia manufaa ya fursa zitakazo tokana na shughuli za uzalishaji, usindikaji, utumiaji na uuzaji wa mazao ya nishati kwa wakulima wadogo kuunganishwa na masoko hasa makampuni ya biashara za kati na ndogo.
 • Tathimini itakayo lenga katika kuangalia uendelevu wa shughuli hizi kwa kuzingatia nguzo tatu za maendeleo endelevu ambapo shughuli hizi ni lazima ziwe na manufaa kiuchumi, kimazingira na kijamii.
 • Mfumo wa upashanaji habari na mafunzo kuhusu nadharia ya uzalishaji na matumizi endelevu ya nishati ya mimea inayo ainisha fursa na changamoto zilizopo utaandaliwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau mbali mbali walio katika sekta hii.

Utafiti

Vichocheo vikubwa kabisa vya kimataifa vinavyochangia katika kushusha tija kwenye sekta ya kilimo kusini mwa jangwa la Sahara ni mabadiliko ya hali ya hewa (Gbetibouo et al 2006.)na mahitaji ya nishati duniani (Von Braun 2007) Ingawaji utabiri wa muda mrefu na muda wa kati wa mahitaji ya nishati duniani haujaweza kutoa makisio ya uhakika lakini hata hivyo kuna kila dalili kwamba inchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara zinaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa.

Nishati ya mimea inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuzipatia jamii zilizopo kusini mwa jangwa la sahara vyanzo mbalimbali vya nishati (mfano, joto, mwanga, kupikia na usafirishaji) pia inaweza kutoa fursa ya kuongeza kipato na kuboresha shughuli za kijamii kama vile elimu.

Hii inaweza kuleta manufaa makubwa kwa wakazi wa maeneo ya vijijini (Umoja wa Mataifa 2007). Hata hivyo, iwapo shughuli za uanzishaji na uendelezaji wa nishati ya mimea hazitafanyika kama inavyotakiwa, zinaweza kuleta athari mbali mbali zikiwemo kuongezeka kwa bei ya chakula na kupungua kwa upatikanaji wa mazao ya chakula (Von Braun 2007), kuondolewa kwa wakulima katika maeneo yenye ardhi ya rutuba kupisha kilimo cha mazao ya nishati, pia athari mbali mbali za kimazingira zinaweza kutokea (Thornton et al 2006.).

Hivyo, mfumo wa nishati mbadala ya mimea kusini mwa jangwa la sahara kuanzia (1) rasilimali za mimea inayotoa nishati (2) mifumo ya usambazaji (3) ubadilishaji na (4) usindikaji wa mazao ya mwisho unatoa fursa za kiuchumi zinazoweza kuwasaidia wakulima masikini waishio vijijini (Leuenberger & Wohlgemuth 2006). Ili kuweza kukabiliana na mabadiliko, maarifa makubwa kwa ajili ya kufanya maamuzi huhitajika (Renn et al 1993); ikiwemo jinsi ya kuongeza faida kwa kuzalisha mazao ya nishati kwa ajili ya masoko ya nje, mchanganyiko madhubuti wa vyanzo vya nishati na upatikanaji wake kwa watumiaji wa nyumbani na viwandani katika maeneo ya vijijini, na mikakati ya kutosha ili kuhakikisha utoshelevu wa chakula (Omamo et al 2006).

Ni elimu/maarifa pekee kuhusu uthamani wa minyororo ya nishati mimea inayozingatia teknolojia za uzalishaji, uwezo wa kitaalam, mazao ya nishati na bidhaa zilizosindikwa kwa kutumia nishati mbadala ndizo zinazoweza kukabiliana na athari za madadiliko ya dunia.

Lengo kubwa ni kuandaa muundo shirikishi wa uchambuzi ambao unaoshirikisha kwa pamoja njia mbali mbali za utafiti ili kutoa mchango katika kusaidia kufanya maamuzi sahihi katika usimamizi wa shughuli za uendelezaji wa mazao ya nishati mbadala. Hii ikiwa na lengo la kutambua athari zinazoweza kujitokeza kwa kutazama hali halisi ya sasa ikilinganishwa na hali inayoweza kujitokeza katika kipindi kijacho. Kwa kuzingatia matokea ya uchambuzi, mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali mbali mbali zinazoweza kujitokeza yatatolewa ili kuweza kuwasaidia wadau waliopo kwenye sekta hii kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Athari zinazoweza kusababishwa na mahitaji ya nishati duniani zitajumuishwa katika tathimini zinazofanyika ikiwa na lengo la kupata taswira ya athari zinazoweza kutokea katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara kutokana na mabadiliko ya mahitaji ya nishati duniani.

Aidha matokeo ya hali ya nishati duniani yanajumuisha mahitaji ya nishati, bei, teknolojia na makisio ya uzalishaji, mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika uzalishaji wa chakula na uzalishaji wa mazao ya nishati.

Tafadhali angali chati iliyopo kwenye ukurasa wa mwanzo.

Matokeo

 1. Mbinu za usanifu elekezi kutoka ngazi za juu hadi za chini duniani zitatumika katika kuanisha matatizo ya nishati, uzalishaji uliokithiri au upungufu utokanao na uzalishaji chini ya kiwango. Mchanganuo huu wa utatuzi utafikiwa kwa matokeo sanifu ya sekta ya kilimo ambayo yatatoa tathimini ya mavuno ya chakula kitaifa kwa nchi za Afrika-kusini mwa jangwa la Sahara inayohusiana na hali ya chakula duniani kwa uchanganuzi wa kati na wa muda mrefu (Von Braun 2007).
 2. Tathmini kuhusu uzalishaji na matumizi ya nishati ya mimea inayolenga katika kubaini ushindani wa kada zitumiazo mazao ya nishati (chakula, malighafi,nishati) na matokea ya rasilimali hizo za mazao ya nishati katika kukidhi mahitaji mengine (chakula, malighafi) na nishati kwa wakati mmoja. Hii italeta uwiano kati ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuunganisha matokea ya tathimini mbili ambapo moja itakuwa inalenga katika kuangalia matokeo ya mahitaji ya nishati duniani kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara na nyingine italenga katika kuangalia ni jinsi gani nchi hizi zinakabiliana na mabadiliko hayo na kutumia fursa zilizopo.
 3. Minyororo thamani ya mazao ya nishati ianziayo katika ngazi ya chini kwa mkulima na kupanda katika ngazi za juu itafanyiwa tathimini kwa njia ya utafiti ili kuweza kuainisha njia sahihi na madhubuti za kuunganisha tija ndogo katika kilimo na masoko hasa makampuni ya biashara ndogo na za kati (SMEs) vijijini ili kuweza kuongeza tija katika sekta ya hiyo ya kilimo.
 4. Tathimini itakayo lenga katika kuangalia uendelevu wa shughuli hizi kwa kuzingatia nguzo tatu za maendeleo endelevu ambapo shughuli hizi ni lazima ziwe na manufaa kiuchumi, kimazingira na kijamii. Tathimini hii pia itachangia katika kutoa taswira ya hali ya upatikanaji wa chakula.
 5. Mfumo wa upashanaji habari na mafunzo kuhusu nadharia ya uzalishaji na matumizi endelevu ya nishati ya mimea inayo ainisha fursa na changamoto zilizopo utaandaliwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau mbali mbali walio katika sekta hii.


Washirika

IFPRI

Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Sera za Chakula (IFPRI) inatafuta ufumbuzi endelevu kwa ajili ya kumaliza njaa na umaskini. IFPRI (Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Sera za Chakula) ni moja kati ya vituo 15 vinavyo fadhiliwa na CGIAR (Kundi la Ushauri la Kimataifa la Utafiti wa Kilimo), ambao ni muungano wa serikali 64 , pamoja na wafadhili binafsi, na mashirika mbali mbali ya kimataifa.http://www.ifpri.org/

Kazi kuu ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Sera za Chakula (IFPRI) katika mradi huu, ni kutoa picha halisi ya mahitaji ya nishati mbadala kimataifa na sera zinazohusu matumizi ya mazao ya nishati na athari zake katika bei za mazao kwenye masoko ya mazao ya kilimo ikiwa ni pamoja na athari zake kwenye matumizi ya ardhi. Kwa kupitia shughuli hii, faida na athari zitokanazo na ukinzani kati ya mazao ya chakula na mazao ya nishati zitafanyiwa tathmini na kutolewa ufafanuzi zikiwemo athari zinazoweza kujitokeza kwa Tanzania.

Ili kuweza kufanya upembuzi wa fursa zitakazo tokana na uanzishaji na undelezeja wa shughuli za kilimo na matumizi ya nishati ya mimea hapa Tanzania na matokeo yake katika masoko ya ndani, tathimini maalum (moduli) itatumika ili kuweza kufahamu muingiliano uliopo kati upatikanaji/uzalishaji na mahitaji ya mazao ya kilimo, ikijumuisha biashara katika ngazi ya kimataifa na kitaifa.

Moduli itakayotumika inaitwa IMPACT ambayo ilibuniniwa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Sera za Chakula (IFPRI) kwa ajili ya kufanya tathimini na utabiri wa upatikanaji/uzalishaji wa chakula, mahitaji ya chakula, na usalama wa chakula mpaka ifikiapo mwaka 2020 na mbele ya hapo.

Kwa kuchanganya tathimini ya sekta za kilimo duniani pamoja na mahitaji na biashara za bidhaa za nishati ya mimea tunalenga katika kupata taswira halisi ya jinsi masoko ya kilimo na nishati yanavyoweza kuathiriwa na aina mbalimbali za uzalishaji wa mazao ya nishati na matumizi yake duniani. Aidha hiyo itafuatiwa na tathimini pana zaidi ili kutoa taswira itakayo onyesha jinsi ambavyo Tanzania inaweza kuathiriwa na muenendo wa masoko ya mazao ya kilimo na nishati duniani na matokeo yake katika mgawanyo wa kipato na matumizi.

Wuppertal Institute

Maendeleo endelevu yanahitaji mbinu jumuishi za kisera na sayansi kwa sababu masuala mengi yajitokezayo hayawezi kutekelezeka ndani ya idara moja au kwa kutumia zana za kisayansi za fani/idara moja. Hapa ndipo tafiti za taasisi ya Wuppertal huanza – programu mbali mbali za utafiti kwa kutumia mitindo ya kifani katika kufanya kazi sambamba na mifumo ya utendaji inayofahamika. Kutumia uendelevu wa kitafiti ndio mtazamo waTaasisi ya Wuppertal uliobainishwa.

Lengo ni kutambua mwenendo wa mifumo ya matumizi ya mazao ya nishati Tanzania kwa ngazi ya kitaifa na kikanda na kutathmini athari zake katika kuongeza uzalishaji wa nishati ya mimea. Aidha hii inatokana na ukweli kwamba mikakati ya uendelezaji wa nishati ya mimea unahitaji kutazama matumizi mengine yaliyopo sasa ya mazao ya nishati. Kwa mfano, chakula na matumizi mengineyo.

Kwahiyo, ni muhimu kufanya tathimini ya mtiririko wa matumizi ya mazao ya nishati ili kuweza kubaini matatizo na fursa zilizopo. Kimsingi, matumizi ya mimea kwa ajili ya malighafi na wakati huo huo kutumika kwa ajili ya nishati baada yakuwa tayari yameshatumika kwa ajili ya malighafi yanaonekana kuwa na matokeo mazuri katika kuongeza tija ya matumizi ya mazao ya mimea kwa ajili ya nishati. Kwa mfano matumizi ya mazao ya nishati kama malighafi na baadae kutumika kwa ajili ya nishati yanaonekana kutoa manufaa zaidi kimazingira na uchumi ukilinganisha na matumizi ya moja kwa moja ambapo mazao hayo hutumika kwa ajili ya nishati pekee. Lengo ikiwa ni kuweka uwiano sawa kati ya matumizi ya mazao ya nishati na matumizi mengineyo kama vile malighafi.

Aidha, hatua ya kwanza ni kubaini matumizi ya nishati ya mimea kwa sasa kwa kuzingatia takwimu za awali zilizopatikana na takwimu zinazopatikana katika kumbukumbu mbalimbali.

Hatua ya pili itakuwa ni kugawanya katika makundi kulingana na matumizi kwa kuzingatia aina mbali mbali za matumizi ya mazao ya nishati ikiwa ni pamoja na kuangali ni jinsi gani mazao hayo yanaweza kutumika kama malighafi na baadae kutumika kwa ajili ya nishati.
Hatua ya tatu ita ainisha athari zinazoweza kutokana na matumizi ya sasa ya mazao hayo ya nishati na fursa zilizopo iwapo mazao hayo yatauzwa katika masoko ya kimataifa. Hii itajumuisha tathimini ya vigezo mbali mbali vinavyohitajika katika kuweka mazingira mazuri kuwawezesha wakulima wadogo kuuza mazao hayo kwemye masoko ya nje. Aidha, matokeo ya tathimini hii yatatumika katika kusaidia kufanya maamuzi sahihi na katika kuwajengea wakulima uwezo wa kushiriki kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutumia fursa zilizopo. http://www.wupperinst.org/

Taasisi ya Uchumi Mazingira na Biashara Duniani (IUW)

Taasisi ya Uchumi, Mazingira na Biashara Duniani (IUW) ni moja kati ya taasisi kadhaa za Kitivo cha Uchumi na uongozi katika Chuo Kikuu cha Leibniz Hannover. Ajenda ya utafiti wa taasisi hii ina jumuisha mada zinazohusiana na mazingira, maendeleo na biashara. Maswali juu ya matumizi ya uwekaji alama kwa bidhaa ziuzwazo nje na athari zake kwa nchi zinazoendelea, kuhusu usalama wa chakula katika biashara, na ushindani wa nchi, au ya utawala wa minyororo thamani katika sekta za kilimo na viwanda ni mifano. Aidha, mkazo umewekwa katika kuchanganua na kutathmini sera za mazingira, kilimo na biashara katika mizani ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Mchango mkubwa wa Taasisi ya Mazingira, Uchumi na Biashara Duniani (IUW) katika mradi ni kuandaa muundo wa ufanyaji tathimini ili kuanisha athari na manufaa ya shughuli za uzalishaji na matumizi ya mazao ya nishati katika ngazi ya kijiji ikiwa ni pamoja na fursa za kuuza mazao hayo nje ya nchi. Aidha modeli itakayotumika (VSAM) pia itajumuisha matumizi ya rasilimali za asili kama vile maji, ardhi, na misitu. Modeli hii itatoa tathimini ya athari na manufaa katika uzalishaji, mgawanyo wa mapato na matumizi, na matokeo yake katika mazingira. Aidha moduli ya VSAM itatumika sambamba na moduli ya CGE, moduli hii ita ainisha mzunguko wa malipo na mapato ulio ainishwa katika moduli ya VSAM ambayo pia itajumuisha masoko ya nje. Aidha, tathimini ya changamoto ni muhimu katika kutoa majibu sahihi ya uwezo wa kaya katika kukabiliana na majanga ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu zaidi.

Vichocheo na vikwazo kwa wakulima wadogo katika shughuli za uzalishaji kwa matumizi ya kaya na uuzaji wa ziada nje ya nchi vitafanyiwa tathimini. Pia katika tathimini hii mikakati madhubuti ya mbinu mbadala za uzalishaji wa mazao ya nishati itabainishwa. Matokeo ya tathimini hii ni kuboreka na kuimarika kwa ujumuishwaji wa shuhguli za uzalishaji wa mazao ya nishati katika mipango ya kilimo bila kusababisha upungufu wa nguvu kazi na ardhi ambayo kwa sasa inatumika katika shughuli za kilimo. Ili kuhakikisha kuna maendeleo endelevu IUW ita fanya tathimini kuhusu jinsi manufaa ya matumizi ya cheti cha ubora wa mazao katika kubaini ubora na kuainisha mapungufu na ubora wa mfumo wa sasa wa mipango ya matumizi ya cheti cha uthibitisho wa ubora wa mazao ikiwa ni pamoja na kutoa mchango wa mbinu bora za uwekaji wa viwango nchini Tanzania.

The Leibniz-Kituo cha Utafiti ardhi tambarare

Umoja wa Taasisi za Utafiti za Leibniz (WGL) una jumuisha taasisi 80. Taasisi zinafanya utafiti kwa kushirikiana na vyuo vikuu, taasisi za biashara na watunga sera za utafiti kuhusu sayansi na matumizi ya tafiti katika ngazi za kimataifa. Kama inavyooneka kwenye nembo, lengo la kituo cha utafiti wa kilimo cha Leibiniz ni kufanya utafiti kuhusu ikolojia ya ardhi inayotumiwa kwa shughuli za kilimo na kubuni mifumo ya matumizi ya ardhi ambayo inakidhi viwango vya kimazingira na ikolojia.

Pamoja na usimamizi wa jumla wa mradi, ZALF itafanya tathimini itakayo lenga katika kuangalia athari na faida baina ya uchumi na mazingira kutokana na uzalishaji, usindikaji na matumizi ya nishati ya mimea. ZALF itafanya tathimini ya athari za kijamii, mazingira na uchumi. Kutokana na matokeo ya utafiti ZALF itatoa mbinu bora kwa serikali, watunga sheria, na wakulima kusini mwa jangwa la sahara zitakazowezesha kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuongeza tija. Pia itaanzisha mfumo utakaowezesha upatikanaji wa habari kuhusu hali halisi ya sasa na athari zinazoweza kujitokeza na maendeleo yanayotarajiwa kupatikana katika nyanja za kiuchumi, kijamii na mazingira katika miaka ijayo.

World Agroforestry Centre (ICRAF)

The World Agroforestry Centre (ICRAF) ni moja ya vituo 15 vya utafiti vilivopo chini ya Kundi la Ushauri la Kimataifa la Utafiti wa Kilimo (CGIR). Malengo ya kituo ni kutoa ujuzi wakisayansi kuhusu manufaa mbalimbali yatokanayo na miti iliyopandwa mashambani na kutumia utafiti wake katika kuboresha sera ambazo zitanufaisha watu wa kipato cha chini na kuboresha mazingira. Ili kuweza kutambua kwamba malengo haya yamefikiwa, hii itabainishwa na kasi ya ongezeko la matumizi ya miti mashambani na ongezeko la matumizi ya mbinu za kilimo zitumiazo miti mashambani, kuongezeka kwa mavuno na tija ya kilimo kwa wakulima wadogo, kupungua kwa umaskini, na kuboreka kwa mazingira.

ICRAF itafanya zoezi la utambuzi wa makundi ya wadau ambao yatajumuisha mchanganyiko kamili wa wadau wa kawaida na mashirika ambayo yanashiriki kwa namna moja au nyingine kwenye shughuli za uzalishaji, usindikaji, biashara ya mazao ya nishati, kutoa mafunzo na kuhamasisha wakulima nk. Pia ICRAF itasimamia shughuli za utekelezaji wa mradi hapa Tanzania ikiwemo kubainisha mahali ambapo mradi wa utafiti utafanyika na kupanga pamoja na kusimamia ukusanyaji takwimu. Lengo likiwa ni kufanya tathimini ya athari zinazotokana na shughuli zote za uzalishaji, usindikaji na utumiaji wa mazao ya nishati kwenye usalama wa chakula, kuingiza kipato, bioanuwai, matumizi ya maji, matumizi ya ardhi na vipingamizi vinavyozuia wakulima wadogo wadogo katika matokeo ya mwisho.

Umoja wa Kuimarisha Utafiti wa Kilimo Mashariki mwa Afrika na Afrika ya Kati (ASARECA)

Ushirika wa kuimarisha utafiti wa kilimo Mashariki mwa Afrika na Africa ya Kati (ASARECA) ni shirika lisilo la kisiasa la Taasisi za Utafiti wa Kilimo za nchi kumi: Burundi, D.R Congo, Writrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Rwanda, Sudan, Tanzania na Uganda. Ushirika unalenga katika kuimarisha na kuongeza tija ya utafiti wa kilimo ili kukuza uchumi, usalama wa chakula, na kuongeza ushindani kwa kilimo cha tija na endelevu.

Kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa kwa kutoa muongozo na msaada katika kuunganisha wataalamu waliobobea na wadau mbali mbali kusini mwa jangwa la sahara. ASARECA itashirikiana na ICRAF katika kuhamasisha mabadiliko ya sera kwa kupitia wadau mbalimbali katika ukanda wa Mashariki mwa Afrika na Afrika ya Kati. Pia itashirika katika kufanya tathimini ya minyororo thamani ya nishati mbadala na hatimaye kueneza mfumo wa habari.

 

better-is better-is better-is better-is better-is better-is
Better-iS © | Designed by Quad-Media